KIPA MBEYA CITY AFUNGIWA MECHI NNE, MENEJA PRISONS APELEKWA KAMATI YA NIDHAMU
SALEH JEMBE / 19 hours ago
Kamati ya nidhamu iliyokutana Januari 1, 2018 ilipitia ripoti mbalimbali za mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Novemba 2, 2017 na ule kati ya Azam FC na Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Chamazi Oktoba 27, 2017.
Kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons, Meneja wa timu ya Tanzania Prisons, Erasto Ntabahani alipelekwa kwenye kamati hiyo ya nidhamu kwa kosa la kumshambulia muamuzi wa akiba.
Kamati imejiridhisha kuwa Ntabahani alimshambulia kwa maneno muamuzi huyo wa akiba na hivyo imemfungia miezi miwili(2) na kulipa faini kwa mujibu wa kanuni ya 40(2) ya udhibiti wa viongozi.
Kamati pia ilipitia suala la golikipa wa Mbeya City, Owen Chaima kudaiwa kumpiga mshambuliaji wa Azam FC Yahya Mohamed.
Chaima alikiri kumpiga Yahya na Kamati kupitia kanuni ya 35(7b) ya udhibiti wa wachezaji imemfungia kucheza mechi 4 na faini.
Visit website
No comments:
Post a Comment