Monday, August 28, 2017

Zaidi ya Tsh. 78 milioni zatafunwa kigoma


Zaidi ya Tsh. milioni 78 zatafunwa Kigoma
28 Aug 2017, 04:00 pm| By Azam News UTAWALA
Halmashauri ya wilaya ya Kigoma imebainika kuwa na matumizi ya fedha yasiyofuata sheria licha ya  kupata hati safi kwa mujibu wa taarifa za  Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali.
Matumizi yaliyobainika ni pamoja na manunuzi  ya shilingi milioni 5 yasiyofuata sheria na malipo ya mishahara takribani milioni 78 kwa watu waliohama vituo vya kazi kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Hayo yamebainishwa na mkaguzi wa mkoa Kassim Mdee katika kikao cha baraza maalumu la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika leo, ambapo madiwani hao wametaka dosari hizo zipatiwe majibu

Mawaziri wa fedha wa nchi 18 kukutana zanzibar septemba 8

Test
Mawaziri wa fedha wa nchi 18 kukutana Zanzibar Sept 8
28 Aug 2017, 06:40 pm| By Jennifer Sumi BIASHARA
Baraza la Mawaziri kutoka Umoja wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika linaloshughulikia Udhibiti Utakasishaji Fedha Haramu, litakutana nchini Tanzania Septemba 08, 2017 katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Visiwani Zanzibar.
Aidha, mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa maafisa waandamizi (makatibu wakuu) utakaofanyika kuanzia Septemba 02 - 06 katika ukumbi wa Hoteli hiyo ya Zanzibar Beach Resort.
Kwa sasa Tanzania ndiuo Mwenyekiti  wa Umoja huo kwa kipindi cha mwaka mmoja, baada ya kupokea Uenyekiti kutoka Jamhuri ya Zimbabwe iliyomaliza muda wake mwezi Agosti, mwaka huu ambapo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. PHILIP ISDOR MPANGO (MB),ndiye mwenyekiti  “President of the Council” atakayeongoza mkutano huo.
Katika mkutano huo pamoja na masuala mbalimbali yatakayojadiliwa, Serikali ya Tanzania, itatumia fursa hiyo  kuwasilisha taarifa ya hatua iliyofikia katika utekelezaji wa mpango wa “Financial Action Task Force” (FATF) ulioasisiwa mwaka 2009.
Mpango huo ulizitaka nchi wanachama kufanya  tathmini ya utekelezaji wa maazimio yaliyoainishwa kwenye FATF, katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya kisheria, kisera, miongozo ya kitaasisi zinazohusisha sekta za fedha na maeneo ya ushirikiano wa kimataifa.
Lengo ni kubaini jinsi nchi wanachama  zilivyojipanga katika kudhibiti suala la utakasishaji fedha haramu na ufadhili wa ugaidi (Anti-money Laundering and Combating the Financing of Terrorism).
Katika mkutano huo, mbinu na mikakati mbalimbali itakayosaidia kudhibiti matatizo hayo zitajadiliwa sanjari na hatua ambayo italeta matokeo chanya na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kufikia maendeleo tarajiwa katika nchi zote wanachama.
Tanzania ni miongoni mwa nchi waanzilishi wa umoja huo ulioasisiwa jijini Arusha,  mwaka 1999, pamoja na  nchi za  Uganda, Kenya, Mauritius, Namibia, Sychelles na Swaziland ambazo zilisaini makubaliano (Memorandum of Understanding - MOU) hayo.
Hatua ambayo ilipelekea Dar es Salaam kutajwa kuwa  makao makuu ya Sekretariati ya Umoja huo wenye nchi wanachama (18) ambazo ni Angola, Botswana, Ethiopia, Kenya, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Rwanda, Afrika Kusini, Swaziland, Sychelles, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Rais magufuli awaongezea mahali takukuru

Test
Rais Magufuli awaongezea makali Takukuru
28 Aug 2017, 07:00 pm| By Jennifer Sumi UTAWALA
Rais John Magufuli amewataka viongozi wa Takukuru nchini kutokuwa na kigugumizi cha kuwachukua hatua wale wote watakaobainika na kuwepo kwa ushahidi wa kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Amesema, hayo alipotembelea makao makuu ya ofisi za taasisi hiyo zilizipo Upanga na kufanya mazungumzo na viongozi na wafanyakazi wake, leo Jumatatu.
“ Kuna mambo mengi ya hovyo yanafanyika, tunahakiki pembejeo za ruzuku na kubaini madai ya bilioni 48 ni hewa,tumebaini zaidi ya wafanyakazi 19,500 ni hewa, tumebaini kaya 56,000 ni hewa zilizopaswa kupata fedha za TASAF, Tumebaini wanafunzi 5,850 waliotakiwa kupatiwa mkopo na kuna vichwa vya treni 11 vimeletwa bila mkataba na mengine mengi, ambayo yanafanyika kwa rushwa. Nataka kuwaona mnachukua hatua zinazostahiki” alisema rais Magufuli.
Rais Magufuli amewataka wafanyakazi wa Takukuru kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu mkubwa na kwamba serikali itafanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Katika mkutano huo wafanyakazi wa taasisi hiyo walimweleza rais Magufuli, matatizo yanayowakabili na kuwaahidi kuyafanyia kazi yakiwemo ya maslahi pamoja na mazingira ya kazi zao.

Friday, August 18, 2017

magazetini leo 19 agosti 2017

Makubwa ya Magazeti ya TZ leo August 19..Udaku, Michezo na Hardnews


Ni asubuhi nyingine tena nakukutanisha na habari kubwa kwenye Magazeti ya Tanzania leo August 19 2017 kuanzia ya Dini, Michezo na Hardnews kujionea yote makubwa yaliyoandikwa.

Uvinza FM