Monday, August 28, 2017

Rais magufuli awaongezea mahali takukuru

Test
Rais Magufuli awaongezea makali Takukuru
28 Aug 2017, 07:00 pm| By Jennifer Sumi UTAWALA
Rais John Magufuli amewataka viongozi wa Takukuru nchini kutokuwa na kigugumizi cha kuwachukua hatua wale wote watakaobainika na kuwepo kwa ushahidi wa kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Amesema, hayo alipotembelea makao makuu ya ofisi za taasisi hiyo zilizipo Upanga na kufanya mazungumzo na viongozi na wafanyakazi wake, leo Jumatatu.
“ Kuna mambo mengi ya hovyo yanafanyika, tunahakiki pembejeo za ruzuku na kubaini madai ya bilioni 48 ni hewa,tumebaini zaidi ya wafanyakazi 19,500 ni hewa, tumebaini kaya 56,000 ni hewa zilizopaswa kupata fedha za TASAF, Tumebaini wanafunzi 5,850 waliotakiwa kupatiwa mkopo na kuna vichwa vya treni 11 vimeletwa bila mkataba na mengine mengi, ambayo yanafanyika kwa rushwa. Nataka kuwaona mnachukua hatua zinazostahiki” alisema rais Magufuli.
Rais Magufuli amewataka wafanyakazi wa Takukuru kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu mkubwa na kwamba serikali itafanyia kazi changamoto zinazowakabili.
Katika mkutano huo wafanyakazi wa taasisi hiyo walimweleza rais Magufuli, matatizo yanayowakabili na kuwaahidi kuyafanyia kazi yakiwemo ya maslahi pamoja na mazingira ya kazi zao.

No comments:

Post a Comment

Uvinza FM