Monday, October 23, 2017

Muungano ni kwa kurahisisha huduma za Bara na visiwani'

'Muungano ni kwa kurahisisha huduma za Bara na visiwani'

23 Oct 2017, 11:05

Kuwepo kwa Taasisi za Muungano Visiwani Zanzibar kunadaiwa kuwa ni suluhisho la kuwezesha na kubainisha kwamba muungano upo na uliwekwa kwa misingi  wa kurahisisha shughuli za wananchi wanaohitaji huduma katika taasisi hizo  kwa pande zote mbili.

Serikali ya Muungano imeendelea kuimarisha taasisi zake hizo na kuhakikisha zinakuwa msadaa na kiunganishi wa wananchi wa Bara na visiwani katika upatikanaji wa huduma bora zinazotolewa na taasisi hizo.

Miongoni mwa taasisi hizo ni pamoja na Uhamiaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na  Kampuni ya simu (TTCL) ambazo kwa kiasi kikubwa zinatoa fursa za ajira kwa wananchi wa pande zote mbili za muungano.

Katika mahojiano maalumu juu ya tathmini ya ziara yake kisiwani Unguja, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba amesema  ziara hiyo imemsaidia kuona taswira mpya na kuahidi kuzifuatilia changamoto alizokutana nazo katika maeneo yote aliyotembelea.

Aidha waziri Makamba amewataka wananchi kuwa na imani na serikali zote mbili ili kufikia maendeleo  yaliyokusudiwa.

Baada ya kumaliza ziara yake kisiwani Unguja, Waziri Makamba anatarajiwa kuendelea na ziara hiyo kisiwani Pemba.

Wednesday, October 18, 2017

Liverpool yairarua Marbior huku Tottenham ikiing’ang’ania Real Madrid

Liverpool yairarua Marbior huku Tottenham ikiing’ang’ania Real Madrid

18 Oct 2017, 01:07am

Klabu ya Liverpool imeibomoa Maribor kutoka Slovenia 7-0 na kuandikisha ushindi mkubwa zaidi wa ugenini kwa vilabu vya uingereza kwenye michuano ya Ulaya.

Washambuliaji Roberto Firmino na Mohammed Salah wote walicheka na nyavu mara mbili, huku Philippe Coutinho, Alex Oxlade-Chamberlain na Trent Alexander-Arnold wakifunga goli moja kia mmoja.

Ilikuwa ni mechi ya kumbukumbu zaidi kwa Chamberlain ambaye amefunga goli lake la kwanza baada ya kuichezea Liverpool mechi nane toka alipoihama Arsenal.  

Ushindi huo wa Liverpool unafunika ushindi mwengine mkubwa kwa timu za Uingereza ikiwemo 6-0 wa Leeds United dhidi ya Lyn kutoka Norway Oktoba 1969, na Manchester United dhidi ya Shamrock Rovers ya Ireland Septemba 1957.

Katika mchezo mwengine, klabu ya Tottenham imelaizimisha sare ya 1-1 dhidi ya Mabingwa Real Madrid katika uga wa Santiago Bernabeu nchini Uhispania.

Spurs walikuwa wa kwanza kupata goli baada ya mshambuliaji Harry Kane kumbabatiza defenda wa Galacticos Raphael Verane kujifunga.  

Real Madrid walisawazisha kabla ya muda wa mapaumziko kwa mkaju wa penalty uliopigwa na Christiano Ronaldo baada ya Toni Kroos kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Kwa upande wa Manchester City wameendeleza makali yao dhidi ya Napoli ya Italia kwa kuwachapa 2-1.

Washambuliaji machachari Raheem Sterling na Gabriel Jesus waliiweka mbele klabu yao kabla ya Amadou Diawara kufunga bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati.

Penati ya Diawara ilikua ya pili kwa Napoli katika mchezo huo, mkwaju wa kwanza ulipotezwa na Dries Mertens.

 

YANGA YA JIPIMA NGUVU NA RHINO RANGERS

Yanga kujipima ubavu kwa Rhino Rangers

18 Oct 2017, 07:53pm

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC leo jioni wanashuka katika dimba la Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora kuumana na Rhino Rangers katika mchezo wa kirafiki.

Mchezo huo ni muhimu kwa Yanga ambao wanajiandaa na mechi ya ligi kuu Tanzania Bara Jumapili hii dhidi ya Stand United, utakaopigwa katika dimba la Kambarage, Shinyanga.

Yanga wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa wametoka kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika dimba la Katiba Bukoba Jumamosi iliyopita.

Kwa upande wao maafande wa Rhino Rangers wanahitaji kuutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi zinazowakabili za ligi daraja la kwanza katika kundi A.

Mchezo huu utakufikia LIVE kupitia Azam Sports 2.

Uvinza FM