Liverpool yairarua Marbior huku Tottenham ikiing’ang’ania Real Madrid
18 Oct 2017, 01:07am
Klabu ya Liverpool imeibomoa Maribor kutoka Slovenia 7-0 na kuandikisha ushindi mkubwa zaidi wa ugenini kwa vilabu vya uingereza kwenye michuano ya Ulaya.
Washambuliaji Roberto Firmino na Mohammed Salah wote walicheka na nyavu mara mbili, huku Philippe Coutinho, Alex Oxlade-Chamberlain na Trent Alexander-Arnold wakifunga goli moja kia mmoja.
Ilikuwa ni mechi ya kumbukumbu zaidi kwa Chamberlain ambaye amefunga goli lake la kwanza baada ya kuichezea Liverpool mechi nane toka alipoihama Arsenal.
Ushindi huo wa Liverpool unafunika ushindi mwengine mkubwa kwa timu za Uingereza ikiwemo 6-0 wa Leeds United dhidi ya Lyn kutoka Norway Oktoba 1969, na Manchester United dhidi ya Shamrock Rovers ya Ireland Septemba 1957.
Katika mchezo mwengine, klabu ya Tottenham imelaizimisha sare ya 1-1 dhidi ya Mabingwa Real Madrid katika uga wa Santiago Bernabeu nchini Uhispania.
Spurs walikuwa wa kwanza kupata goli baada ya mshambuliaji Harry Kane kumbabatiza defenda wa Galacticos Raphael Verane kujifunga.
Real Madrid walisawazisha kabla ya muda wa mapaumziko kwa mkaju wa penalty uliopigwa na Christiano Ronaldo baada ya Toni Kroos kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Kwa upande wa Manchester City wameendeleza makali yao dhidi ya Napoli ya Italia kwa kuwachapa 2-1.
Washambuliaji machachari Raheem Sterling na Gabriel Jesus waliiweka mbele klabu yao kabla ya Amadou Diawara kufunga bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati.
Penati ya Diawara ilikua ya pili kwa Napoli katika mchezo huo, mkwaju wa kwanza ulipotezwa na Dries Mertens.
No comments:
Post a Comment