Yanga kujipima ubavu kwa Rhino Rangers
18 Oct 2017, 07:53pm
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC leo jioni wanashuka katika dimba la Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora kuumana na Rhino Rangers katika mchezo wa kirafiki.
Mchezo huo ni muhimu kwa Yanga ambao wanajiandaa na mechi ya ligi kuu Tanzania Bara Jumapili hii dhidi ya Stand United, utakaopigwa katika dimba la Kambarage, Shinyanga.
Yanga wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa wametoka kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika dimba la Katiba Bukoba Jumamosi iliyopita.
Kwa upande wao maafande wa Rhino Rangers wanahitaji kuutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi zinazowakabili za ligi daraja la kwanza katika kundi A.
Mchezo huu utakufikia LIVE kupitia Azam Sports 2.
No comments:
Post a Comment