Thursday, September 21, 2017

RONALDO AREJEA BERNABEU NA KICHAPO, REKODI MPYA YAWEKWA KWA REAL MADRID

RONALDO AREJEA BERNABEU NA KICHAPO, REKODI MPYA YAWEKWA KWA REAL MADRID
/ 60 minutes ago

Mshambuliaji wa Real madrid ambaye ni mchezaji bora wa dunia Cristiano Ronaldo jana Usiku alikuwa na wakati mgumu wakati aliporejea dimbani kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza kifongo cha kutocheza michezo mitano.

Ikiwa Nyumbani Santiago Bernabeu Real madrid walijikuta wakifungwa bao la dakika za mwisho na kupoteza mchezo huo kwa bao 1-0 toka kwa Wageni Real Betis

Licha ya kushambulia na kukosa nafasi nyingi za wazi kwa muda wote wa mchezo Real Madrid walishindwa kabisa kufunga bao na kupelekea kuvunjwa rekodi yao ya kufunga goli kila mechi wanayocheza kwa takribani michezo 73 mfululizo mara ya mwisho kushindwa kufunga ikiwa ni misimu miwili iliyopita katika mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City.

Licha ya kutengeneza nafasi zaidi ya 25 katika mchezo huo safu ya ushambuliaji ya Real madrid ikiongozwa na Ronaldo haikuweza kupata bao lolote.


Emmanuel Martin yuko tayari kwa ajili ya Ndanda

EMMANUEL MARTIN YUKO TAYARI KWA AJILI YA NDANDA
/ 16 minutes ago

Kiungo Emmanuel Martin yuko tayari kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Ndanda FC.

Mshambulizi huyo ambaye aliumia katika mechi iliyopita dhidi ya Majimaji ya Songea, amerejea mazoezini tokea juzi na jana tulikutaarifu.

Lakini leo ameendelea na mazoezi na inaonekana yuko tayari kwa ajili ya mechi hiyo itakayopigwa katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, keshokutwa.

TCRA yasema Online TV zimerahisisha maisha


TCRA yasema, 'Online TV' zimerahisisha maisha
20 Sep 2017, 08:29 pm|
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa nchi imepiga hatua na kuwa ya mfano wa kuigwa baada ya ongezeko kubwa la ‘Online tv’ ambazo zimekuwa na faida kubwa ikiwemo kuongeza ajira pamoja na kuhabarisha umma kwa haraka zaidi kupitia sekta ya mawasiliano.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, leo Jumatano, Kaimu Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa TCRA, Semu Mwakyanjala amesema kwa sasa kuna ongezeko la watumiaji wa mtandao (Internet) wanaokadiriwa kufikia milioni kumi na nane (milioni 18) kutoka milioni tano katika mwaka 2011.
“Kwa sasa watumiaji wameongezeka zaidi hadi kufikia milioni 18, sasa humu kuna tv nyingine za mtandaoni ‘Online TV’, kutuma miamala ya simu kwa kutumiana pesa na mambo mengine ikiwemo mitandao ya kijamii kama WhatsApp na mengine,” alieleza Mwakyanjala.
Hata hivyo akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari kuhusiana na uwepo wa wingi wa tv za mtandaoni ‘Online tv’ kama ni tishio kwa usalama wa Mawasiliano?, Kaimu meneja huyo alikanusha mfumo huo kuwa tishio bali una faida nyingi zaidi.
"Mtu unaweza usiwe nyumbani kwako ila unaweza kuangalia tv, Popote upo barabarani unatakiwa kupata taarifa ‘up-to-date’  Yaani ni moja wapo ya mambo ambayo Serikali yetu imefanikiwa kuwaletea maendeleo wananchi wake kwani nchi nyingine hakuna hivi vitu."
Hata hivyo amesema, athari huenda zikawepo iwapo watu watatumia vibaya huduma hiyo.
Kuhusu baadhi ya faida zake, Mwakyanjala amesema, sekta hiyo kwa sasa imeongeza ajira na kuwa chachu ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi.
Alisema hayo wakati wa kutoa taarifa kwa umma kuhusu ufahamu wa matumizi sahihi na salama ya mitandao ya kompyuta na Intaneti, ambapo aliweka wazi kuwa, kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao nchini (TZ-CERT) kimepewa jukumu  la Kitaifa la kuratibu matukio ya usalama katika mitandao ya kompyuta na Intaneti kwa kushirikiana na vyombo vingine  vikiwemo vya kikanda na kimataifa katika kusimamia matukio ya usalama mitandaoni.
“TZ-CERT ilianzishwa kwa sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010, kifungu namba 124. Kifungu  namba 5(1) cha kanuni za mawasiliano ya kielektroniki na Posta na kuzinduliwa rasmi 2015. Hivyo chombo hichi kina majukumu mengi ikiwemo kufuatilia shughuli za kiusalama mitandaoni hii ni pamoja na kutoa ushauri wa kiusalama wa kukabiliana na masuala ya kiusalama. Kufanya uchambuzi na kutoa miongozo ya kitaalamu kwa umma na wadau na mambo mengine,” alieleza Mwakyanjala.

Tuesday, September 19, 2017

SPORTPESA YAELEZA NIA YA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUUKARABATI UWANJA WA TAIFA KWA AJILI YA FAINALI ZA AFCON 2019

SPORTPESA YAELEZA NIA YA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUUKARABATI UWANJA WA TAIFA KWA AJILI YA FAINALI ZA AFCON 2019



Kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ya SportPesa Limited Ijumaa Septemba 13, 2017 imefanya mkutano na waandishi wa Habari kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhusiana na zoezi linaloendelea la ukarabati wa Uwanja wa Taifa uliopo Temeke, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugezi wa Utekelezaji na Utawala wa SportPesa Tanzania, Bwana Tarimba Abbas amesema; “Tunashirikiana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha uwanja huu unakamilika kwani tumetafuta wataalamu ambao wamebobea katika fani hii kuhakikisha uwanja wetu unakuwa katika ubora wa kimataifa.

Kuelekea kwenye fainali za AFCON za vijana mwaka 2019 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji kwa mara ya kwanza, uwanja wa Taifa ambao ni miongoni mwa viwanja vikubwa na bora barani Afrika, utakuwa katika hali nzuri ikiwa ni sehemu ya maandalizi muhimu kuelekea kwenye fainali hizo.

Sisi kama SportPesa lengo letu kuu ni kuendeleza sekta ya michezo nchini Tanzania tukianzia na Mpira wa Miguu na kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tunaamini tutafanikiwa kwa asilimia zaidi ya mia moja.

Naye Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bwana Yusuph Singo ameongeza kuwa; Tunawashukuru na tunawapongeza sana kwani kuendesha michezo sio lelemama. Kuendesha michezo ni jambo kubwa na linahitaji uwekezaji mkubwa na inahitaji pesa nyingi. Kwahiyo tunapopata wenzetu wakatusaidia, kwanza sisi kama serikali ni kuwashukuru na pia ni kufanya nao kazi kwa karibu sana.

SportPesa kwa kweli wameonesha mfano, wamejitahidi sana kudhamini vilabu mbalimbali, wametusaidia kurekebisha uwanja na kama sikosei gharama za kurekebisha uwanja zimefika takribani bilioni 1.3, ni hela nyingi sana hivyo sisi tunawashukuru na tunaendelea kuwaomba wasikate tamaa.

Kampuni ya SportPesa ambayo inajihusisha na michezo ya kubashiri nchini ndiyo mdhamini mkuu wa vilabu vya Simba, Yanga na Singida United huku ikiwa imejidhatiti katika kuhakikisha sekta ya michezo nchini inapata hadhi yake inayostahili.

Saturday, September 16, 2017

Mabasi 9 yapigwa faini kwa mwendokasi nyakati za usiku

Mabasi 9 yapigwa faini kwa mwendo kasi nyakati za usiku
16 Sep 2017, 11:12 am|
Mabasi saba ya abiria yamekamatwa  na kutozwa faini kwa kosa la mwendokasi na kutofuata sheria za usalama barabarani huku wakihatarisha maisha ya abiria.
Kamatakamata hiyo  ambayo imesimamiwa na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani, Fotunatus  Muslim akiwa na timu ya viongozi na askari  Mkoa wa Morogoro imefanyika usiku wa kuamkia leo, Jumamosi.
Zoezi la ukamataji mabasi hayo limefanyika eneo la Dumila, Wilaya ya Kilosa mkoani hapa, na lilichukua takribani saa mbili ambapo mabasi hayo yamezuiwa kuondoka hadi asubuhi huku yakitozwa faini.
Kamanda Muslim amesema jeshi hilo halitakubali kuona maisha ya watanzania yakipotea  kutokana na uzembe wa baadhi ya madereva.
Amesema  kikosi hicho cha usalama barabarani kimeahidi kupambana na madereva wa mabasi ya abiria hususan nyakati za usiku kwani ndiyo wamekuwa wakiendesha kwa mwendokasi huku wakidai  serikali muda huo inakuwa imelala.
Mabasi ya abiria zaidi ya saba yanayofanya safari kati ya mkoa wa Mara (Musoma), Dar es salaam na Mwanza - Dar es salaam yamekaguliwa na kutozwa faini.
Muslim amesema  madereva wengi wamekuwa wakifuata sheria za barabarani nyakati za mchana kwa kuhofia kukamatwa kutokana na tochi zilizopo na inapofika nyakati za usiku madereva hao wamekuwa wakitumia mwanya huo kuendesha kwa mwendo kasi.
Akizungumzia dhamira ya Polisi, Muslim amesema ni kuwalinda raia na mali zao na kuwataka askari wa usalama barabarani kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
amesema operesheni hiyo ni endelevu na sasa itakuwa kwa nchi nzima kwa usiku na mchana huku akiwataka madereva hao kuacha kudanganyika kwa madai kuwa tochi usiku hazifanyi kazi.
"Nimekuja na slogani ya Kamata hii ni kwa wale madereva wasiotii na kufuata sheria na tutapambana nao kila wakati na nyakati zote na hiyo itasaidia abiria kusafiri salama na matumizi ya barabarani kuwa bora," amesema kamanda Muslim
Mmoja wa abiria aliyejitambulisha kwa jina la Leon Mwete, aliyekuwa katika moja ya basi yaliyokamatwa eneo hilo la Dumila amesema zoezi hilo ni zuri na linafaa kuendelea.
Amesema hii itapunguza ajali za barabarani na kwamba kwa sasa uendeshaji wa madereva wengi ni mzuri ukilinganisha na zamani.

Yanga yapania pointi 3 leo

Yanga yakamia pointi 3 Songea
16 Sep 2017, 12:03 pm|
Mzunguko wa tatu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), unaendelea leo kwa viwanja vitano kuwaka moto huku mabingwa watetezi Yanga SC ambao wako Songea wakizikodolea macho point tatu za Majimaji.
Kwa mujibu wa ratiba ya VPL, leo Jumamosi Septemba 16, 2017 Majimaji FC ya Songea itacheza na  Young Africans ya Dar es Salaam, saa 10.00 jioni katika Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Mbao imesafiri hadi Manungu mkoani Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar wakati Tanzania Prisons ya Mbeya itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC kwenye Uwanja wa Sokoine.
Lipuli FC itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting katika Uwanja wa Samora, Iringa wakati Stand United itacheza na Singida United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Tuesday, September 12, 2017

Friday, September 8, 2017

Hatimae mh.lissu azinduka


Dkt.Kashinji : Lissu amezinduka na anaendelea vizuri Nairobi
08 Sep 2017, 01:58 pm| By Jennifer Sumi MAISHA
Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vicent Mashinji, amesema kuwa mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu ambaye jana alishambuliwa kwa risasi  mjini Dodoma na baadaye kupelekwa mjini Nairobi, Kenya, amezinduka na anaendelea vizuri.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mashinji amesema kuwa ameongeza na Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe na kumuhakikishia kuwa Mjumbe huyo wa kamati kuu ya chama amezinduka na anaendelea vizuri baada ya sindano alizochomwa kwaajili ya kupumzika na safari kwisha.
Dkt. Kashinji amesema, damu ya Lissu ilimwagika kabla ya wakati na hivyo kuwataka makamanda na wanachama wote kwenda katika hospitali na zahanati kwaajili ya kujitolea damu.
“Tuchangie damu ili kuwe na damu za kutosha ili ziweze kusaidia wenye uhitaji,” alisema Dkt. Kashinji.
Kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa Lissu, Dkt. Kashinji amesema halijawatisha bali limewaimarisha.
Naye Makamu wa Mwenyekiti wa Chadema Bara, Profesa Abdalla Safari, amesema wao kama wanasheria linapotokea suala la kupigwa risasi kama lililomtokea Lissu huangalia mambo makubwa mawili, imetumika silaha gani na amepigwa eneo gani, hivyo Lissu alilengwa kupigwa kifuani na kichwani hivyo walikusudia kumuua.
“Hali hii inatia simanzi , wana usalama wafanye kazi yao kwa weledi kulibaini hili,” alisema Prof Safari.
Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amesema, Kazi ya Serikali ni kulinda usalama wa raia, hivyo kama imeshindwa kufanya hivyo basi kuna kasoro katika uwajibikaji.
“Kwa sisi tuliokuwa kwenye uongozi kwa muda mrefu, uwajibikaji unaweza kukosekana kwa makusudi au kwa uwezo na kupanga,” alisema Sumaye

Uvinza FM