Yanga yakamia pointi 3 Songea
16 Sep 2017, 12:03 pm|
Mzunguko wa tatu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), unaendelea leo kwa viwanja vitano kuwaka moto huku mabingwa watetezi Yanga SC ambao wako Songea wakizikodolea macho point tatu za Majimaji.
Kwa mujibu wa ratiba ya VPL, leo Jumamosi Septemba 16, 2017 Majimaji FC ya Songea itacheza na Young Africans ya Dar es Salaam, saa 10.00 jioni katika Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Mbao imesafiri hadi Manungu mkoani Morogoro kucheza na Mtibwa Sugar wakati Tanzania Prisons ya Mbeya itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC kwenye Uwanja wa Sokoine.
Lipuli FC itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting katika Uwanja wa Samora, Iringa wakati Stand United itacheza na Singida United kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Saturday, September 16, 2017
Yanga yapania pointi 3 leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Uvinza FM
-
Uvinza fm Leo tumekua na ugeni wa Mwanasheria kutoka BAK-AIDS KIGOMA Bi.MWAJABU MASHAKA Pamoja na Msaidizi wa kisheria Bw.JOSEPH L KANY...
No comments:
Post a Comment