TCRA yasema, 'Online TV' zimerahisisha maisha
20 Sep 2017, 08:29 pm|
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa nchi imepiga hatua na kuwa ya mfano wa kuigwa baada ya ongezeko kubwa la ‘Online tv’ ambazo zimekuwa na faida kubwa ikiwemo kuongeza ajira pamoja na kuhabarisha umma kwa haraka zaidi kupitia sekta ya mawasiliano.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, leo Jumatano, Kaimu Meneja wa Mawasiliano kwa Umma wa TCRA, Semu Mwakyanjala amesema kwa sasa kuna ongezeko la watumiaji wa mtandao (Internet) wanaokadiriwa kufikia milioni kumi na nane (milioni 18) kutoka milioni tano katika mwaka 2011.
“Kwa sasa watumiaji wameongezeka zaidi hadi kufikia milioni 18, sasa humu kuna tv nyingine za mtandaoni ‘Online TV’, kutuma miamala ya simu kwa kutumiana pesa na mambo mengine ikiwemo mitandao ya kijamii kama WhatsApp na mengine,” alieleza Mwakyanjala.
Hata hivyo akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari kuhusiana na uwepo wa wingi wa tv za mtandaoni ‘Online tv’ kama ni tishio kwa usalama wa Mawasiliano?, Kaimu meneja huyo alikanusha mfumo huo kuwa tishio bali una faida nyingi zaidi.
"Mtu unaweza usiwe nyumbani kwako ila unaweza kuangalia tv, Popote upo barabarani unatakiwa kupata taarifa ‘up-to-date’ Yaani ni moja wapo ya mambo ambayo Serikali yetu imefanikiwa kuwaletea maendeleo wananchi wake kwani nchi nyingine hakuna hivi vitu."
Hata hivyo amesema, athari huenda zikawepo iwapo watu watatumia vibaya huduma hiyo.
Kuhusu baadhi ya faida zake, Mwakyanjala amesema, sekta hiyo kwa sasa imeongeza ajira na kuwa chachu ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi.
Alisema hayo wakati wa kutoa taarifa kwa umma kuhusu ufahamu wa matumizi sahihi na salama ya mitandao ya kompyuta na Intaneti, ambapo aliweka wazi kuwa, kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao nchini (TZ-CERT) kimepewa jukumu la Kitaifa la kuratibu matukio ya usalama katika mitandao ya kompyuta na Intaneti kwa kushirikiana na vyombo vingine vikiwemo vya kikanda na kimataifa katika kusimamia matukio ya usalama mitandaoni.
“TZ-CERT ilianzishwa kwa sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010, kifungu namba 124. Kifungu namba 5(1) cha kanuni za mawasiliano ya kielektroniki na Posta na kuzinduliwa rasmi 2015. Hivyo chombo hichi kina majukumu mengi ikiwemo kufuatilia shughuli za kiusalama mitandaoni hii ni pamoja na kutoa ushauri wa kiusalama wa kukabiliana na masuala ya kiusalama. Kufanya uchambuzi na kutoa miongozo ya kitaalamu kwa umma na wadau na mambo mengine,” alieleza Mwakyanjala.
Thursday, September 21, 2017
TCRA yasema Online TV zimerahisisha maisha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Uvinza FM
-
Uvinza fm Leo tumekua na ugeni wa Mwanasheria kutoka BAK-AIDS KIGOMA Bi.MWAJABU MASHAKA Pamoja na Msaidizi wa kisheria Bw.JOSEPH L KANY...
No comments:
Post a Comment