Friday, September 8, 2017

Hatimae mh.lissu azinduka


Dkt.Kashinji : Lissu amezinduka na anaendelea vizuri Nairobi
08 Sep 2017, 01:58 pm| By Jennifer Sumi MAISHA
Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vicent Mashinji, amesema kuwa mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu ambaye jana alishambuliwa kwa risasi  mjini Dodoma na baadaye kupelekwa mjini Nairobi, Kenya, amezinduka na anaendelea vizuri.
Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mashinji amesema kuwa ameongeza na Mwenyekiti wa Chama, Freeman Mbowe na kumuhakikishia kuwa Mjumbe huyo wa kamati kuu ya chama amezinduka na anaendelea vizuri baada ya sindano alizochomwa kwaajili ya kupumzika na safari kwisha.
Dkt. Kashinji amesema, damu ya Lissu ilimwagika kabla ya wakati na hivyo kuwataka makamanda na wanachama wote kwenda katika hospitali na zahanati kwaajili ya kujitolea damu.
“Tuchangie damu ili kuwe na damu za kutosha ili ziweze kusaidia wenye uhitaji,” alisema Dkt. Kashinji.
Kuhusu tukio la kupigwa risasi kwa Lissu, Dkt. Kashinji amesema halijawatisha bali limewaimarisha.
Naye Makamu wa Mwenyekiti wa Chadema Bara, Profesa Abdalla Safari, amesema wao kama wanasheria linapotokea suala la kupigwa risasi kama lililomtokea Lissu huangalia mambo makubwa mawili, imetumika silaha gani na amepigwa eneo gani, hivyo Lissu alilengwa kupigwa kifuani na kichwani hivyo walikusudia kumuua.
“Hali hii inatia simanzi , wana usalama wafanye kazi yao kwa weledi kulibaini hili,” alisema Prof Safari.
Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amesema, Kazi ya Serikali ni kulinda usalama wa raia, hivyo kama imeshindwa kufanya hivyo basi kuna kasoro katika uwajibikaji.
“Kwa sisi tuliokuwa kwenye uongozi kwa muda mrefu, uwajibikaji unaweza kukosekana kwa makusudi au kwa uwezo na kupanga,” alisema Sumaye

No comments:

Post a Comment

Uvinza FM