Wednesday, April 4, 2018
Wednesday, March 28, 2018
Leo tumekua na ugeni wa Mwanasheria kutoka BAK-AIDS KIGOMA Bi.MWAJABU MASHAKA
Pamoja na Msaidizi wa kisheria Bw.JOSEPH L KANYABWOYA kutoka UVINZA PARALEGAL FOUNDATION(UPAFO) UVINZA.Wamezungumzia sheria ya ndoa ya 1971 kwa kuchambua kwa kina:-
a.Aina za ndoa
b.Taratibu za kufunga ndoa
c.Sifa za kufunga ndoa
d.Haki za mwanamke katika ndoa
e.Dhana ya ndoa.
Tegea sikio redio yako pendwa kesho alhamisi tar.29.3.2018 saa 10:30 jioni upate kujua mengi kupitia 96.5 mhz
Thursday, March 8, 2018
Tuesday, February 13, 2018
NAIBU WAZIRI WA HABARI SANAA NA MICHEZO JULIANA SHONZA AMEWATAKA WAANDISHI WA HABARI WAFANYE KAZI KWA KUZINGATIA USAWA NA HAKI KATIKA KUANDIKA HABARI.
Wednesday, February 7, 2018
IFIKAPO SAA SAA 8:00-9:30 ALASIRI NI KIPINDI CHA AFRICAN FIRE
Kipndi hewani AFRICAN FIRE na uvinza fm kwanzia saa 8:00-9:30 alasili
Hatua1.historia ya FRANCO saa8:00-8:30 mchana
Hatua ya mwisho.nyimbo halisi za kiafrika saa 8:30-9:30
Utakua nami:HUSSAIN
Piga simu au utume sms 0788 941 947
Pia mitandao ya kijamii I
Kwa Facebook page:96.5 uvinza fm community radio au @uvinzafm02
Instagram uvinzafm
Twitter @uvinzafm2
WhatsApp 0788 941 947
Pia tusikilize online http//Mixlr.com/uvinza-fm
Kwa blog yet www. Uvinzafm.blogspot.com
WAANDISHI WA HABARI NA WATANGAZAJI WA RADIO ZA JAMII WAMETAKIWA KUZINGATIA MAADILI NA KANUNI ZA UANDISHI WA HABARI.
Waandishi wa
habari watangazaji kutoka redio Jamii wametakiwa kufanya kazi kwa
Kuzingatia maadili ya uandishi wa habari.
Haya yamezungumzwa na Mkufunzi wa redio za kijamii MWL ROSE HAJI kutoka shirika la Kimataifa la elimu Sayansi Utamaduni (UNESCO)Katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za kijamii kuhusu uwaandaaji wa habari na vipindi bora katika ukumbi wa wakala wa Majengo Mjini dodoma.
Mwl ROSE amesema mwandishi anaezingatia maadili ya uandishi anatakiwa kufanya kazi bila upendeleo.
Friday, January 5, 2018
KIPA MBEYA CITY AFUNGIWA MECHI NNE, MENEJA PRISONS APELEKWA KAMATI YA NIDHAMU SA
KIPA MBEYA CITY AFUNGIWA MECHI NNE, MENEJA PRISONS APELEKWA KAMATI YA NIDHAMU
SALEH JEMBE / 19 hours ago
Kamati ya nidhamu iliyokutana Januari 1, 2018 ilipitia ripoti mbalimbali za mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Novemba 2, 2017 na ule kati ya Azam FC na Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Chamazi Oktoba 27, 2017.
Kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons, Meneja wa timu ya Tanzania Prisons, Erasto Ntabahani alipelekwa kwenye kamati hiyo ya nidhamu kwa kosa la kumshambulia muamuzi wa akiba.
Kamati imejiridhisha kuwa Ntabahani alimshambulia kwa maneno muamuzi huyo wa akiba na hivyo imemfungia miezi miwili(2) na kulipa faini kwa mujibu wa kanuni ya 40(2) ya udhibiti wa viongozi.
Kamati pia ilipitia suala la golikipa wa Mbeya City, Owen Chaima kudaiwa kumpiga mshambuliaji wa Azam FC Yahya Mohamed.
Chaima alikiri kumpiga Yahya na Kamati kupitia kanuni ya 35(7b) ya udhibiti wa wachezaji imemfungia kucheza mechi 4 na faini.
Visit website
Thursday, November 16, 2017
Ndugu mpenzi msikilizaji ifikapo saa 11:30-11:45 jion nikipindi cha Mazingira kinachofadhiriwa na UNESCO
Ndugu mpenzi msikilizaji ifikapo saa 11:30-11:45 jion nikipindi cha Mazingira kinachofadhiriwa na UNESCO
Tupe maoni yako
kwa sms 0788 941 947
WhtsApp 0788 941 947
Twitter @uvinzafm2
Kwa Facebook page 96.5 Fm community Radio
Pia tusikilize online kwa blog yet www.uvinzafm.blogspot.com
Link Uvinza fm is on Mixlr http://mixlr.com/uvinza-fm
Monday, October 23, 2017
Muungano ni kwa kurahisisha huduma za Bara na visiwani'
'Muungano ni kwa kurahisisha huduma za Bara na visiwani'
23 Oct 2017, 11:05
Kuwepo kwa Taasisi za Muungano Visiwani Zanzibar kunadaiwa kuwa ni suluhisho la kuwezesha na kubainisha kwamba muungano upo na uliwekwa kwa misingi wa kurahisisha shughuli za wananchi wanaohitaji huduma katika taasisi hizo kwa pande zote mbili.
Serikali ya Muungano imeendelea kuimarisha taasisi zake hizo na kuhakikisha zinakuwa msadaa na kiunganishi wa wananchi wa Bara na visiwani katika upatikanaji wa huduma bora zinazotolewa na taasisi hizo.
Miongoni mwa taasisi hizo ni pamoja na Uhamiaji, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Kampuni ya simu (TTCL) ambazo kwa kiasi kikubwa zinatoa fursa za ajira kwa wananchi wa pande zote mbili za muungano.
Katika mahojiano maalumu juu ya tathmini ya ziara yake kisiwani Unguja, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba amesema ziara hiyo imemsaidia kuona taswira mpya na kuahidi kuzifuatilia changamoto alizokutana nazo katika maeneo yote aliyotembelea.
Aidha waziri Makamba amewataka wananchi kuwa na imani na serikali zote mbili ili kufikia maendeleo yaliyokusudiwa.
Baada ya kumaliza ziara yake kisiwani Unguja, Waziri Makamba anatarajiwa kuendelea na ziara hiyo kisiwani Pemba.
Wednesday, October 18, 2017
Liverpool yairarua Marbior huku Tottenham ikiing’ang’ania Real Madrid
Liverpool yairarua Marbior huku Tottenham ikiing’ang’ania Real Madrid
18 Oct 2017, 01:07am
Klabu ya Liverpool imeibomoa Maribor kutoka Slovenia 7-0 na kuandikisha ushindi mkubwa zaidi wa ugenini kwa vilabu vya uingereza kwenye michuano ya Ulaya.
Washambuliaji Roberto Firmino na Mohammed Salah wote walicheka na nyavu mara mbili, huku Philippe Coutinho, Alex Oxlade-Chamberlain na Trent Alexander-Arnold wakifunga goli moja kia mmoja.
Ilikuwa ni mechi ya kumbukumbu zaidi kwa Chamberlain ambaye amefunga goli lake la kwanza baada ya kuichezea Liverpool mechi nane toka alipoihama Arsenal.
Ushindi huo wa Liverpool unafunika ushindi mwengine mkubwa kwa timu za Uingereza ikiwemo 6-0 wa Leeds United dhidi ya Lyn kutoka Norway Oktoba 1969, na Manchester United dhidi ya Shamrock Rovers ya Ireland Septemba 1957.
Katika mchezo mwengine, klabu ya Tottenham imelaizimisha sare ya 1-1 dhidi ya Mabingwa Real Madrid katika uga wa Santiago Bernabeu nchini Uhispania.
Spurs walikuwa wa kwanza kupata goli baada ya mshambuliaji Harry Kane kumbabatiza defenda wa Galacticos Raphael Verane kujifunga.
Real Madrid walisawazisha kabla ya muda wa mapaumziko kwa mkaju wa penalty uliopigwa na Christiano Ronaldo baada ya Toni Kroos kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Kwa upande wa Manchester City wameendeleza makali yao dhidi ya Napoli ya Italia kwa kuwachapa 2-1.
Washambuliaji machachari Raheem Sterling na Gabriel Jesus waliiweka mbele klabu yao kabla ya Amadou Diawara kufunga bao la kufutia machozi kwa mkwaju wa penati.
Penati ya Diawara ilikua ya pili kwa Napoli katika mchezo huo, mkwaju wa kwanza ulipotezwa na Dries Mertens.
YANGA YA JIPIMA NGUVU NA RHINO RANGERS
Yanga kujipima ubavu kwa Rhino Rangers
18 Oct 2017, 07:53pm
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara, Yanga SC leo jioni wanashuka katika dimba la Ally Hassan Mwinyi mkoani Tabora kuumana na Rhino Rangers katika mchezo wa kirafiki.
Mchezo huo ni muhimu kwa Yanga ambao wanajiandaa na mechi ya ligi kuu Tanzania Bara Jumapili hii dhidi ya Stand United, utakaopigwa katika dimba la Kambarage, Shinyanga.
Yanga wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa wametoka kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Kagera Sugar katika dimba la Katiba Bukoba Jumamosi iliyopita.
Kwa upande wao maafande wa Rhino Rangers wanahitaji kuutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi zinazowakabili za ligi daraja la kwanza katika kundi A.
Mchezo huu utakufikia LIVE kupitia Azam Sports 2.
Uvinza FM
-
Uvinza fm Leo tumekua na ugeni wa Mwanasheria kutoka BAK-AIDS KIGOMA Bi.MWAJABU MASHAKA Pamoja na Msaidizi wa kisheria Bw.JOSEPH L KANY...